Breaking News

TAEC YAHAMASISHA WASICHANA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

 





Na Suzana Alex

Mkuu wa  Kanda ya kati tume ya nguvu za atomu Tanzania(TAEC) ,Machibya Matulanya amewahasa watoto wakike kusoma masomo ya sayansi kwani masomo hayo hutoa nafasi za kufanya kazi katika taasis ya mionzi kama wataalamu.

Akizungumza  kwenye  mahafali ya kidato cha nne(4)yaliyofanyika katika Viwanja vya Dodoma Sekondari iliyopo Jijini Dodoma Septemba 25, alipokua akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa tume ya nguvu za atom Tanzania prof.Najat Mohamed amesema taasis hiyo inahamasisha wanafunzi walioko mashuleni hasa wasichana kusomea zaidi masomo ya kisanyansi

"Ninawashauri  wanafunzi kusoma masomo ya sayansi fikrieni kusoma zaidi fani zinazohusiana na nishati,afya,mazingira na teknolojia ya Habari na utafiti kutokana na kuwa mataifa tajiri yaliyoendelea duniani yamewekeza zaidi kwenye maeneo hayo,"amesema 

Pia ameahaidi kushirikiana na Dodoma Sekondari  kutatua changamoto ya maktaba ya kisasa inayoikumba shule hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa tume ya nguvu za atom Tanzania prof. Najat Mohamed ametoa kianzio cha sh. million Moja ambayo itafika hapa shuleni kwaajili ya kuhalikisha tunaanza mchakato wa kuondoa changamoto ya maktaba ya kisasa katika shule hii. 

Changamoto ya ukosefu wa maktaba ya kisasa naahidi kuifikisha sehemu inayostahiki lakini baada ya kuifikisha sehemu hiyo naahidi kwamba taasis yetu itafanya kazi bega Kwa bega na sehemu ambayo tutakua tumeifikisha changamoto hiyo ili kuhakikisha kwamba changamoto hii inamalizika kabisa,"amesema Matulanya