Breaking News

Banda la BERGER PAINTS INTERNATIONAL LTD lang'ara Katika Maonyesho ya Wahandisi



Na Hawa Ismail- Dar es Salaam 

Katika maonyesho ya wahandisi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, kampuni ya BERGER PAINTS INTERNATIONAL LTD imevutia wengi kupitia banda lao lililojaa ubunifu na bidhaa bora za kisasa.

Meneja wa Miradi, Bw. Obed Machoka, amesema kampuni hiyo inazalisha aina mbalimbali za rangi zinazotumika katika mazingira tofauti ikiwemo:

- Rangi za majumbani

- Rangi za viwandani

- Rangi za barabarani (road marking)

- Rangi za meli

- Rangi za mbao

- Rangi za sakafu

Aidha, Bw. Machoka aliongeza kuwa katika maonyesho hayo, kampuni imewasilisha pia rangi za paa, mabwawa ya kuogelea (swimming pool), pamoja na rangi maalum kwa viwanja vya michezo kama _basketball_.

 “Tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa pamoja nasi, na tunawaalika waendelee kutembelea banda letu ili wajionee ubora wa bidhaa zetu,” alisema Bw. Machoka.

Kwa upande wake, Afisa Masoko, _Bi. Halima Rajab_, alieleza kuwa maonyesho haya ni fursa ya kipekee kwa BERGER PAINTS kuonyesha ubora wa bidhaa zao ambazo zinapatikana kote nchini, katika mikoa yote.

Bi. Halima alisisitiza kuwa mteja anaweza kupata huduma moja kwa moja kutoka ofisini, bila usumbufu.

Kwa wateja wanaotaka kutembelea ofisi, BERGER PAINTS INTERNATIONAL LTD wanapatikana Temeke–Chang’ombe, mtaa wa Mbozi Road,


 _Plot No. 38_, karibu na Chuo cha VETA Keko. Vilevile, huduma zinapatikana kupitia mitandao ya kijamii kwa jina @bergerpaints.tz.