MWAKAGENDA AINADI VYEMA ILANI YA CCM NYANDA ZA JUU KUSINI.
Katika muendelezo wa mikutano ya kampeni nchini, Mjumbe wa kamati ya ushindi ya chama cha mapinduzi UWT katika mikoa ya nyanda za juu kusini ambaye pia ni mbunge mstaafu Mhe.Sophia Mwakagenda ameendelea kuwanadi wagombea mbalimbali katika mikoa hiyo ya Nyanda za juu kusini ambapo safari hii tarehe 24 Sept.2025 amemnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Mhe.Bahati Ndingo hii yote ni katika kutafuta kura za Rais, Wabunge na madiwani katika mikoa ya Njombe, Mbeya na Songwe ikiwa ni ziara zake za kuanzia Vitongoji kata kwa kata hadi majimbo ili kukipa ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.



