Breaking News

JOHN THE BAPTIST SEKONDARI YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE -2026

Mgeni Rasmi na Mbunge wa Viti Maalum Taifa, Dkt. Catherine Canute Joachim, akikabidhi vyeti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist, jana, Septemba 5, 2026.

Rasmi na Mbunge wa Viti Maalum Taifa, Dkt. Catherine Canute Joachim, akikabidhi akiteta jambo na  Mwenyekiti wa Board wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist, Murungi Kichwabuta jana, Septemba 5, 2026.

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam 

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist, iliyopo Boko Basihaya jijini Dar es Salaam, imefanya mahafali ya wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne kwa mwaka 2023/2027, huku ikiendelea kutoa elimu bora pamoja na malezi yenye misingi ya bweni kwa wanafunzi wake.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007, imekuwa ikiendesha mahafali mbalimbali na kushuhudia mafanikio ya wahitimu wake katika elimu na maisha kwa ujumla.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mgeni Rasmi na Mbunge wa Viti Maalum Taifa, Dkt. Catherine Canute Joachim, ameipongeza shule hiyo kwa juhudi zake za kutoa elimu kwa wasichana na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika kuboresha elimu, hususan elimu ya wasichana.

Dkt. Joachim amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka msisitizo katika kuboresha elimu na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa watoto wa kike, huku akieleza kuwa shule binafsi na wadau wengine wana nafasi muhimu katika kuunga mkono juhudi hizo.

John The Baptist Secondary School, iliyopo Boko Basihaya jijini Dar es Salaam, inaendelea kujitangaza kuwa chaguo sahihi kwa wazazi wanaolenga kuwapatia watoto wao wa kike elimu bora pamoja na malezi yanayozingatia misingi bora ya mazingira ya bweni.