Na Mwandishi wetu Dar es Salaam
Kampuni ya inayotoa huduma ya kuwatafutia Ajira vijana kwa wewekezajiji nchi inatarajia kuwatafutia vijana zaidi ya elfu kumi Ajira katika kipindi Cha MWAKA 2025 -2030.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji Tanzania TISEZA Mkurugenzi Mtendaji wa OPTIMUM GROUP Bw. STEVEN MZUMA Amesema Vijana watakaopata fursa ya kupata Ajira ni wote ambao wana Elimu ya kati, Elimu ya juu, mafundi pamoja na wabeba mizigo.
"Vijana wenye Elimu na wasio na Elimu pia wote tunawatafutia Ajira Bora wawe Wana uwezo wa kujituma hata kama hawajasoma na mpaka Sasa tumewatafutua kazi vijana zaidi ya elufu tatu 3,000 na lengo letu ifikapo 2030 tuwe tuwe tuwapatia Ajira Vijana elfu kumi 10,000 , Alisema Bw. MZUMA
Aidha Amesema huduma za Uwekezaji wa Ajira kwa Vijana zinapatikana Viwandani, Migodini na kwenye Miradi mbalimbali nchini.
UZINDUZI WA BODI YA TISEZA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 28, 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi ya TISEZA pamoja na mwongozo kwa wawekezaji ambapo ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inataka kujenga uchumi jumuishi, shindani na wenye mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 28, 2025 wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya TISEZA na Mwongozo kwa wawekezaji
DAR ES SALAAM
SERIKALI imezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), pamoja na Mwongozo wa Watoa Huduma kwa Wawekezaji (ISPs), hatua inayoashiria mwanzo wa mageuzi mapana katika sekta ya uwekezaji nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 28, 2025, wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema uzinduzi wa bodi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inataka kujenga uchumi jumuishi, shindani na wenye mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji.
Waziri Mkumbo amebainisha kuwa TISEZA, iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi ya 2025, ndio chombo kikuu cha kuratibu na kuendeleza uwekezaji nchini, ikichukua nafasi ya TIC na EPZA zilizounganishwa.
Amesema TISEZA inapaswa kuwa injini ya kutafsiri maono ya Dira 2050 katika kuvutia wawekezaji, kuboresha mazingira ya biashara na kuijenga Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu bora barani Afrika kwa urahisi wa kufanya biashara.
“Jukumu la TISEZA ni kubadilisha ndoto za Taifa kuwa vitendo. Mwekezaji akifika TISEZA anatakiwa kumaliza changamoto zake zote hii ndiyo maana ya huduma mahala pamoja,” amesisitiza.
Akizungumzia fursa kwa vijana, Waziri Mkumbo ametangaza mikakati mipya ya kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Kituo Maalum cha Wawekezaji Vijana (Youth Investors Resource Centre) kitakachotoa mafunzo, ushauri na uwezeshaji kwa vijana wanaotaka kuwekeza.
Pili ni kuwa na Programu ya Taifa ya Uwekezaji wa Viwanda kwa Vijana, ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya ardhi kwa vijana wanaomaliza vyuo kuanzisha viwanda. Maeneo yaliyotengwa ni Dodoma (Nala, ekari 100), Pwani (Kwala, ekari 20), Mara (Bunda, ekari 100), Ruvuma (Songea, ekari 100) na Bagamoyo (ekari 20).
Matukio mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya TISEZA na Mwongozo kwa wawekezaji