ZAN TIMIZA YALETA UKOMBOZI WA UWEKEZAJI KWA WATANZANIA
Na Hawa Ismail-Dar es Salaam
Mfuko wa uwekezaji wa Zan Timiza umeelezwa kuwa fursa mpya inayolenga kuwawezesha Watanzania, hususan wanawake ambao wamekuwa wakipoteza fedha kupitia mifumo isiyo rasmi ya vijumbe, kuwekeza kwa njia salama na kupata gawio kutokana na fedha zao.
Akizungumza kuhusu fursa hiyo, Baba Levo amesema mwananchi anaweza kuanza kuwekeza kwa kiasi cha Shilingi 20,000 na kupata gawio linalokadiriwa kuwa kati ya asilimia 13 hadi 15, huku akiwataka wananchi kutumia mifumo inayotambulika kisheria badala ya kuwaweka fedha zao kwa watu wasio na uhakika.
Amesema kupitia Zan Invest, mwekezaji anaweza kupakua programu hiyo kwenye simu yake na kufanya uwekezaji moja kwa moja, huku akiwa na uwezo wa kuchagua mfuko anaoutaka kulingana na muda anaotaka kupata gawio.
Aidha, amesema kuna mifuko mbalimbali ikiwemo ya mwisho wa mwaka na ya kila baada ya miezi mitatu, ambapo hisa moja ni Shilingi 100 na kiwango cha kuanzia kuwekeza ni Shilingi 20,000.
Baba Levo amesema uwepo wa huduma hiyo unalenga pia kuwasaidia wananchi kudhibiti changamoto zinazowakabili kupitia mifumo isiyo rasmi ya vijumbe, akieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipoteza fedha zao au kucheleweshewa malipo.
Amesema Zan Timiza ni miongoni mwa mifuko iliyowekwa kwa lengo la kutoa fursa ya uwekezaji wa hadi mwaka mmoja, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kuchagua mifuko inayotambulika kisheria.
Ameeleza kuwa yeye mwenyewe amewahi kutumia mfumo wa vijumbe na kukumbana na changamoto, ikiwemo kucheleweshewa fedha, jambo lililomsukuma kuhamasisha wananchi kutumia njia rasmi za uwekezaji.
Aidha, amesema huduma hiyo inalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwamba baada ya kuanza na matumizi ya simu janja, huduma za USSD zitawezesha hata wenye simu za kawaida kushiriki katika uwekezaji.pia amesema wanapatikana kwa simu namba 0750011250



