Breaking News

TBS YAIMARISHA UDHIBITI WA UBORA WA BIDHAA

 



Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam 

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa bidhaa nchini kupitia ukaguzi, usajili wa bidhaa na utoaji wa vyeti kwa wazalishaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, amesema hatua hizo zimeongeza uwezo wa wazalishaji, hususan wajasiriamali wadogo, kufikia viwango vinavyowawezesha kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Oktoba 27, 2026, jijini Dar es Salaam, Dkt. Katunzi amesema TBS imeandaa viwango 3,901 vya bidhaa na kutoa vyeti na leseni za ubora 3,940 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2026.

Amesema shirika hilo pia limewekeza katika kuboresha miundombinu ya huduma, ikiwemo ujenzi wa ofisi na maabara za Viwango House katika Dodoma na Mwanza, huku maandalizi ya ujenzi wa kituo kama hicho yakiendelea Arusha.

Amesema uwekezaji huo unalenga kusogeza huduma za upimaji karibu na wananchi, kuongeza ufanisi wa ukaguzi na kuhakikisha bidhaa zinazofika sokoni zinakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa walaji.