FRV. SAID MNDEME ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU WA T
Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua FRV. Said Mndeme kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Kabla ya uteuzi huo, Mndeme alikuwa akihudumu kama Mkurugenzi wa Miliki katika Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), nafasi iliyompa uzoefu katika usimamizi wa masuala ya miliki za wakala huo.
Mndeme anachukua nafasi ya Bw. Daud Kandoro, ambaye amemaliza muda wake wa utumishi katika nafasi hiyo.
Uteuzi huo unamuweka Mndeme katika nafasi ya kusimamia shughuli za wakala huo, unaohusika na masuala ya majengo ya Serikali na usimamizi wa miliki zake
.
