TEAM USHINDI FOUNDATION WACHANGIA DAMU NA KUFANYA USAFI HOSPITALI AMANA
Taasisi ya Team Ushindi Mkoa wa Dar es Salaam wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa lengo la kuchangia Damu nakufanya usafi wa mazingira.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mwenyekiti wa Team Ushindi Foundation Taifa Bw. Mussa Njite amesema kuwa Taasisi hiyo inathamini suala la utunzaji mazingira na kuokoa maisha ya Kina mama, watoto na watu wengine ambao wanahitaji kuongezewa damu hivyo wamekuwa wakijitolea kuchangia damu na kuhamasha wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa wingi.
“Team Ushindi Foundation, Mkoa wa Dar Es Salaam inapenda kuungana na wananchi wengine kujitolea kushiriki shughuli za usafi na uchangiaji damu ili kuunga mkono jitihada za hospitali za kuhudumia wananchi wanaofika kupata huduma”Amesema Bw.Njite
![]() |







