MAKONDA ASHIRIKI UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA PAMOJA YA AFCON 2027
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb.), ameshiriki utiaji saini wa hati ya makubaliano ya pamoja ya nchi waandaji wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027.
Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha uratibu, ushirikiano na maandalizi ya pamoja kati ya Tanzania, Kenya na Uganda kuelekea mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.
Aidha, Mhe. Makonda anatarajiwa kushiriki ziara ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, katika nchi waandaji wa AFCON 2027.
