Breaking News

DOTTO MAGARI RASMI BALOZI WA KAMPUNI YA IZO MOTOR COMPANY LTD BETRI ZA DRAYA ZISIZOTUMIA MAJI

 


Na Mwandishi  wetu 

Kampuni ya Izo Motor's Company LTD leo imezindua bidhaa mpya ya betri "Izo Battery "ambayo haitumii maji kwa ajili ya kuchaji ikiwa na ubora unaodumu kwa muda mrefu.

Aidha kampuni hiyo inayopatikana Kariakoo,Narung'ombe na Limumba Jijini Dar es salaam,imekuja wakati sahihi ikiwa ni kutoa Suluhu ya upatikanaji wa mabetri ya magari yenye ubora kwa bei nafuu nchini.

Akizungumza leo Mei 12,2026 wakati wa uzinduzi wa betri hiyo balozi wa bidhaa hiyo mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni Dotto Magari amesema kuwa betri hiyo haitumii maji,bali inatumia draya hivyo mteja akinunua anapewa waranti wa miaka mitano.

Aidha amesema kutokana na hali nzuri ya uwekezaji iliyopo nchini kampuni hiyo ya wazawa imeamua kuwekeza katika utenegenezaji wa Betri hizo nakutengenza ajira kwa Watanzania pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Ameongeza kuwa,kwa sasa wanazo aina mbalimbali za betri katika saizi tofauti zinazokidhi mahitaji  ya magari aina mbalimbali, ambapo bidhaa hizo zinapatikana kwa bei nafuu jumla na reja reja.

"Kampuni ya "Izo battery"imeingia makubaliano na mimi kuwa balozi wake kwani kupitia ushirikiano huu naamini bidhaa hizi zitaendelea kuwafikia Watanzania wengi zaidi pamoja na masoko ya kimataifa huku ubora wetu ukiendelea kujenga imani kubwa kwa watumiaji"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Izo Motor's Company Ltd Bw.Izo Mahenge amesema kuwa betri hizo zimetengenezwa katika kiwango cha ubora mkubwa,kutokana na ushindani wa kibiashara uliyopo.

"Izo Battery zinazalishwa hapa Tanzania,ni betri bora na imara,watumiaji wa magari wazitumie "Izo Battery" hawatajuta kuzitumia popote walipo."Amesema Mahenge

Nakuongeza kuwa"kwenye kiwanda chetu tumeajiri watu wengi sana zaidi ya watu 60,tuna mawakala zaidi ya 70 nchi nzima,wote wanasambaza hizi betri,tumekuja na vitu vya tofauti.