MILIKI UBUNIFU YAENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MAENDELEO YA TAIFASIKU YA MILIKI UBUNIFU DUNIANI 2026 DR. MLYUKA APEWA TUZO
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Siku ya Miliki Ubunifu Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Aprili 26 ili kuongeza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu wa Miliki Ubunifu (IP) na kuhimiza ubunifu katika nyanja mbalimbali. Maadhimisho ya siku hii yalianzishwa na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) mwaka 2000 ili kutambua mchango wa wabunifu kote ulimwenguni.
Nchini Tanzania, Aprili 26 ya kila mwaka inaambatana na sikukuu ya kitaifa ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
Kwa Tanzania Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wameadimisha siki Siku ya Miliki Ubunifu Duniani mey 8,2026 jijini Dar es Salaam.
Lengo la maadhimisho haya ni kujenga uelewa wa umma juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na Miliki Ubunifu pamoja na kutoa elimu kuhusu sheria, kanuni na miongozo inayosimamia nyanja mbalimbali za Miliki Ubunifu.
Miongoni wa waliopewa Tuzo hizo ni Dr.Erasto Mlyuka, kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo ametunukiwa tuzo ya heshima katika Maadhimisho ya Siku ya Miliki Ubunifu Duniani 2026 kwa niaba ya Taasisi hiyo, yaliyoandaliwa na Business Registrations and Licensing Agency (BRELA).
Tuzo hiyo ilitolewa jana ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, kwa kutambua mchango wake mkubwa katika ubunifu, uwekezaji na maendeleo ya biashara nchin aliuzuria hafla hiyo.
Kwa mwaka 2026 kaulimbiu ni: “MILIKI UBUNIFU NA MICHEZO: JITAYARISHE, JIPANGE, VUMBUA”
Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuangalia mchango wa Miliki Ubunifu katika michezo.
Makundi ya Tuzo zitakazotolewa ni pamoja na: • Patent Excellence Award
• Brand Protection Excellence Award
• Young Innovator Achievement Award
• Copyright Achievement Award
• Outstanding Woman Entrepreneur in Trademark Use Award

