Breaking News

MBUNGE KISANGI AKIHUDHURIA KIKAO KAZI CHA MPANGO MIKAKATI WA MAENDELEO WA MIAKA KUMI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU NYERERE KIBAHA

 

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mariam Nassoro Kissangi akichangia mada wakati aliposhiriki ufungaji wa Kikao kazi cha Mpango Mkakati wa vipaumbele vya  Maendeleo kwa kipindi cha Miaka Kumi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kilichofanyika Tarehe 18, Februari 2026 Katika Ukumbi wa mihadhara WA Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Mhe.Kisangi akichangia mada alianza kuipongeza Serilkari kupitia Manispaa ya Temeke kwa kuandaa Kikao kazi  na kuwapa Mafunzo ya uandaaji Mpango Mkakati wa vipaumbele vya Maendeleo kwa kipindi cha Miaka Kumi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuwa Mafunzo hayo yatawawezesha kuwa chachu na kufanya kazi kwa ufanisi na uanda mpana  wa kuelewa vipaumbele vya Mpango Mkakati wa Maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.



Aidha Mbunge Kisangi aliwataka Wabunge, Mstahiki Meya, Naibu Meya, Mkurugenzi, Madiwani na wakuu wa Idara kuwa na umoja na mshikamano Katika kuelekea utekelezaji wa mpango wa Maendeleo wa Miaka Kumi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke 







Kikao kazi hicho kilifungwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Uzairu Abdul Athumani