MSTAHIKIMEYA UZAIRU ADHAMILIA KULETA MAENDELEO MAKUBWA WILAYANI TEMEKE
Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Mstahikimeya Manispaa ya Temeke Mhe. Uzairu Athumani amedhamilia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya, Elimu, Uchumi na miundombinu wilayani Temeke.
Hayo yamejiri mara baada ya baraza la madiwani kupitisha bajeti kubwa ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 193 ambayo haijawahi kupitishwa toka kuanzishwa kwa halmashauri hiyo.
Aidha Meya Uzairu amesema bajeti hiyo inakwenda kukidhi mahitaji ya kiuchumi, kiafya na kielimu kwa wananchi wa Temeke ambapo hospitali kubwa mbili na shule kubwa za ghorofa zaidi ya 5 zinakwenda kujengwa kupitia bajeti hiyo



