URUSI INASEMA HAKUNA MAENEO YA POLAND YALIYOLENGWA KUSHAMBULIWA
Wizara ya ulinzi ya Urusi inasema haikupanga kushambulia maeneo yoyote nchini Poland, baada ya Warsaw kusema ndege 19 zisizo na rubani za Urusi ziliingia kwenye anga yake wakati wa mashambulizi ya usiku magharibi mwa Ukraine.
Katika taarifa za kila siku kuhusu vita vya Ukraine, imesema: "Hakuna maeneo ya Poland yaliopangwa kulengwa.
"Masafa ya juu zaidi ya ndege za UAV zilizotumika katika shambulizi [huko Ukraine] hayazidi kilomita 700 [maili 435].
"Hata hivyo, tuko tayari kufanya mazungumzo na wizara ya ulinzi ya Poland kuhusu suala hilo."