MAAFISA WAKAGUZI NA ASKARI WA MAKAO MAKUU YA POLISI ZANZIBAR WAFANYA MATEMBEZI MAENEO MBALIMBALI MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wameungana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama katika Matembezi ya Pamoja yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Matembezi hayo yalilenga kujenga afya na kuendelea kujenga mshikamano na mashirikiano miongoni mwa vyombo hivyo vyenye jukumu la kudumisha amani, usalama na utulivu nchini.
Matembezi hayo yalihusisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar, Kikosi cha Mafunzo, Kikosi cha Zimamoto na Uokozi, Jeshi la Kujenga Uchumi na Kikosi cha Valantia Zanzibar.




