UFANISI WA UBUNIFU VETA WAONGEZEKA
Na. Wellu Mtaki , Dodoma
Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepiga hatua kwenye Ubunifu wa vifaa mbalimbali ikiwemo matumizi ya Nishati ya Umeme na Jua , vifaa vya matumizi ya Kilimo vya umwagiliaji pamoja na Ubunifu wa mitindo .
Hayo amebainisha Mwenyekiti wa Bodi ya VET Prof. Sifuni Ernest Mchome wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitembelea Banda la VETA nakujionea vifaa mbalimbali ambavyo vinapatikana kwenye banda hilo na kuonesha Kuwa VETA imepiga hatua kubwa kwenye Ubunifu.
Aidha amesema kuwa Elimu inayopatikana VETA ni chachu kubwa kwa maendeleo ya kijana kujiinua kiuchumi hivyo Amewataka wananchi kupeleka watoto wao kupata Elimu hiyo
Sambamba na hayo amewaasa wadau wa mfumo wa VET pamoja na ya mfumo wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA )kwa vitu wanavyovibuni kwa sasa wavifanye kwa ukubwa zaidi ili kuleta tija nchini.
Ikumbukwe kuwa VET ni bodi inayojihusisha na masuala ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania na inakuwa sehemu ya VETA ambapo kwa pamoja zinasaidia watanzania kupata Elimu ya ufundi na hatimaye kuajiriwa au kujiajiri .

