Breaking News

MKALAMA YAJA NA MAONESHO YA MBEGU BORA YA VITUNGUU



 Na.  Wellu Mtaki, Dodoma 

Afisa Ugani  Mifugo halmashauri ya Wilaya ya Mkalama  Mkoani Singida Joseph Maiko  amebainisha kuwa mbegu aina ya  Red Mang'ola  ni mbegu Bora kwa wakulima wa vitunguu kwani inauwezo wa  kukomaa kwa siku 120 lakini uzalishaji wake ni mkubwa na inauwezo wa kupata gunia 80 Hadi 100 kwenye hekari Moja.

Hayo yamebainishwa  Agost 1 ,2025 wakati akizungumza na Nico media Katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma mara baada ya Uzinduzi wa maonesho Hayo yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Philipo Isidore Mpango huku akieleza mazao ambayo wanaonesha ni pamoja na zao la vitunguu, Alzeti na Mtama Sambamba na Mifugo aina ya Ng'ombe kuku na Samaki aina ya kambale.

Amesema uzalishaji wa vitunguu kwa almashauri ya Mkalama imeweza kusaidia kukuza uchumi wa Mkoa Singida pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja wa halmashauri hiyo.

Aidha amesema kuwa wapo wataalam wabobevu ambao wataweza kusaidia Mkulima kupata Elimu ambayo itamnufaisha kupata uwelewa mkubwa kuhusu kilimo hicho pamoja na upatikanaji wa mbegu hizo.

Sambamba na hayo amesema kuwa halmashauri hiyo imejikita Katika ufugaji wa samaki aina ya kambale, pamoja kuku wa kienyeji  huku akieleza mbegu ya kuku wa asili inapatikana.



Pia amewasihi watanzania watembelee Katika Banda hilo Ili kupata Elimu itakayo msaidia mkulima na Mfugaji kufuga na kulima kilimo cha tija.