Breaking News

Jasdeep Singh Babhra Awekeza kwa Jamii: Vyumba vya Wazazi, Maktaba na Bima kwa Mamia



Na mwandishi wetu

Mtia nia wa jimbo la Temeke, Jasdeep Singh Bahbra amesema kuwa amewekeza fedha zake binafsi katika miradi mbalimbali ya kijamii yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi, hususan sekta ya elimu na afya.

Akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Jasdeep alieleza kuwa amejenga vyumba nane vya kujifungulia katika wodi ya wazazi kwa ajili ya kina mama, huku pia akijenga jiko katika shule za msingi ambalo linahudumia takribani watoto 1,500 bila mchango wowote kutoka kwa wazazi.

Aidha, amesema amejenga maktaba kwa ajili ya shule ya sekondari ili kusaidia wanafunzi katika kujisomea na kukuza elimu yao.

Katika hatua nyingine, Jasdeep alifichua kuwa kupitia ufadhili wa ubalozi wa Marekani, amefanikisha ugawaji wa kadi za bima ya afya kubwa kwa kaya 77, sawa na watu 560, hatua inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Mbali na jitihada hizo, Jasdeep alipongeza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuonesha dira thabiti ya maendeleo ya mwaka 2050, akisema inatoa msingi wa kuwapata viongozi waadilifu, wawazi, wachapa kazi na wenye kuleta maendeleo katika jamii.