HALIMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA IMELENGA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Afisa ugani kilimo Halmashauri ya wilaya ya Singida Emanuel Ambrose amesema ushiriki wao kwenye maonesho ya wakulima (nane nane) yamelenga kutoa Elimu Kwa wakulima ili kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Amesema kuwa kwenye vipando vyao wamehusika mazao ya Alizeti,vitunguu pamoja na Mtama ambayo ni Mazao ya kibiashara Mkoani Singida.
ambrose ameyasema hayo Agosti 1, 2025 wakati anazungumza na Nico Media Jijini Dodoma Katika maonesho nane nane .
Aidha amefafanua kuwa ukuaji wa Mazao hayo ya kitunguu, Alizeti pamoja na Mtama ambao kwa upande wa Alizeti pamoja na vitunguu huchukua siku 90 mpaka kuwa tayari kwa mavuno wakati Mtama ukichukua miezi 6.
Hata hivyo Afisa huyo amewaasa Wananchi wanaotembelea maonesho hayo ya nane nane wafike katika mabanda yao ya kilimo ili waweze kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo kwa ajili ya kuongeza thamani ya kilimo chao.
