TFSRP HAJA NA UVUMBUZI WA KUBORESHA MIFUMO YA IKOLOJIA
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Program ya mifumo himilivu ya chakula (TFSRP) kupitia maonesho ya 32 ya wakulima (Nanenane) imelenga kutoa Elimu kuhusu Kuimarisha uvumbuzi na Kuboresha maarifa na mifumo ya ikolojia inayohusiana na kuongeza usambazaji wa teknolojia za kilimo himilivu na mifumo ya tahadhari katika kilimo.
Akieleza Afisa habari wa Program hiyo Nyabaganga Taraba Agosti 2,2025 wakati akizungumza na Nico Media katika Banda la maonesho ya nanenane Jijini Dodoma huku akisema kuwa Program hiyo inatekelezwa Kwa muda wa miaka mitano(5) kuanzia 2023/2024 mpaka 2027/2028 ikitekelezwa na Wizara ya Kilimo Tanzania Bara na Visiwani.
Hata hivyo alieleza kuwa Program hiyo Inafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mfuko wa maendeleo ya Afrika (IDA) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300 sawa na takribani bilioni 756 za Tanzania.
Sambamba na Hayo alibainisha kuwa lengo la Program hiyo ni kuongeza ufanisi ,kuleta matokeo chanya na uwekezaji wa rasilimali za Umma na masuala ya kisera.
Pia amesema kuwa program hiyo inatekeleza vipaumbele vya mpango wa kuendeleza Sekta ya kilimo awamu ya pili sehemu ya mazao ikiwemo, ununuzi wa vifaa vya kupima afya ya udongo, ujenzi wa nyumba za maafisa ugani,ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na shughuli mbalimbali.
