MIKOPO NAFUU YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAPATIKANA EQUITY BANK
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Katika kuhakikisha wakulima wa mazao ya mboga mboga na wafugaji wa maziwa wanatunza mazao Yao na kuongeza thamani ili yasiharibike kwa haraka kampuni ya Bajaj processpack campany Limited kwa kushirikiana na Equity Bank wamesaini mkataba utakaowezesha kuwasaidia wakulima na wafugaji kupata Mkopo wa vifaa kwa ajili ya kutunzia mazao Hayo.
Hayo ameyasema Mkurugezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kondoa Shabani Millao wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusainiana Mkataba huo huku akiwasihi wakulima na wafugaji kufika Katika benki za Equity popote Tanzania na kujipatia fursa itakayosawasaidia kujiinua kiuchumi.
Aidha Millao ameeleza kuwa utunzaji wa mazao hayo kwa vifaa vya kisasa na Bora itasaidia kuwepo kwa mabadiliko ya bei na kupunguza hasara ambayo itakwamisha Katika kuendelea kuzalisha bidhaa zingine.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Kilimo biashara wa Equity Benki Teofora Madilu amesema kuwa Benki inachangia kukuza uchumi wa mkulima na Mfugaji mdogo mdogo kwa kumpa Mkopo nafuu utakaowezesha kutunza mazao yake na kuongeza thamani, Sambamba na kupata soko kubwa kwa watumiaji wa mazao Katika soko la ndani na nje kwa ujumla.

