Breaking News

MAZITO ALIYOKUTANA NAYO MKUU WA WILAYA YA CHAMWINO ALIPOTEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS




 Na. Wellu Mtaki, Dodoma .

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja  amewataka wananchi kutembelea  banda  la ofisi ya makamu wa Rais Ili  kupata Elimu juu ya Muungano pamoja na  kutambua fursa zilizopo Katika ofisi hiyo.


Amezungumza hayo leo Agosti 4,2025 Jijini Dodoma kwenye viwanja vya maonesho ya nanenane wakati alipotembelea banda hilo huku akisisitiza vijana na wanawake kutambua fursa na kufanyia kazi fursa zilizopo kwenye ofisi hiyo.


  "kuwa ukija kwenye banda hilo unaweza kujifunza mambo mbalimbali ya Muungano kwa sababu wakati mwingine Kuna mambo yanazungumzwa ya nakuwa hayana uhalisia Wala usahihi" amesema.


Aidha ameeleza  kuwa  ipo miradi ambayo inatolewa na Ofisi hiyo ambayo inamuwezesha Vijana na Wanawake kupewa mashine na vitendea kazi ambayo vitawezesha kupata kipato.




"Pia kwa vijana Kuna fursa miradi ambayo inatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais  na uwezeshwaji unafanya kwa vijana na wanawake kwa kupewa mashine na vitendea kazi mbalimbali ya kupata kipato na kuchangia kwenye uchumi ngazi ya familia , ngazi ya halmashauri na ngazi ya taifa" amesema.


Sambamba na hayo  mafanikio ya Muungano wa ofisi ya Makamu wa Rais imefanikiwa kujenga Diplomasia na uhusiano wa Nchi na Nchi kikanda na kimataifa  na kufanya Tanzania kuwa mstari wa mbele Katika kudumisha na kuimarisha ujirani mwema na uhusiano Mzuri na Nchi za Afrika na Dunia kwa ujumla.


Pia huduma za kijamii ususani ujenzi wa Madarasa , vituo vya afya,zahanati , Miradi ya maji , Miradi ya kupunguza umasikini na utoaji wa haki zimeimarika kutokana na Miradi iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa pande zote za Muungano.




Ikumbukwe kuwa maonesho ya nanenane yalizinduliwa Agost 1 ,2025 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. philip Isidore Mpango na kubebwa na kauli mbiu isemayo " Chagua viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo na Ufugaji na Uvuvi 2025".