COOP BENKI NA AGTIF WAMEKUBALIANA KUWEZESHA MKOPO KWA VIJANA WAKULIMA
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Naibu katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Stephen Nindi amewasihi vijana na wanaushirika ambao watanufaika wa mkopo wenye thamani ya Shilingi za kitanzania bilioni 8.5 kuwa na taratibu za kuweka marejesho ili kuwezesha mkopo huo Kuwa endelevu.
Yamezungumzwa hayo Agosti 4,2025 jijini Dodoma katika viwanja vya maonesho ya nanenane wakati wa hafla ya makubaliano ya kuwezesha utoaji mikopo kati ya Benki ya ushirika Tanzania (Coop Benki) kwa kushirikiana na mfuko wa pembejeo ( AGTIF)
Pia amewata watengeneza Mfumo Imara wa kufatilia fedha pindi zinapokopeshwa na kulejeshwa lli kusaidia kurudisha kwa wakati pamoja na kusaidia kuongea kipato na uzalishaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa pembejeo (AGTIF) Itandula Gambalagi amebainisha kuwa taasisi yake tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 94 tangu kuanzishwa kwake huku akieleza kuwa mfuko wa pembejeo za kilimo ulianzishwa chini ya Sheria ya mfuko wa pembejeo za kilimo,sura ya 401 marekebisho ya mwaka 2002 kwa lengo la kupunguza pengo la usambazaji wa pembejeo za kilimo.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Coop Benki Godfrey Ng'urah amesema kuwa makubaliano ya Benki ya ushirika Tanzania (Coop Benki) kwa kushirikiana na mfuko wa pembejeo ( AGTIF) ni kwa ajili ya kutoa mkopo wenye thamani ya Shilingi bilioni 8.5 kwa vijana wanaojihusisha na kilimo kupitia program ya Jenga kesho iliyo Bora(BBT).
Ikumbukwe kuwa maonesho ya 32 ya nanenane inabebwa na kauli mbiu isemayo " Chagua viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo , Ufugaji na Uvuvi 2025".


