UTENDAJI BORA UMEWAFANYA TPDC KUIBUKA NA TUZO MARA TANO MFULULIZO
Na Hawa Ismail, Saba Saba
Mkuu wa kitengo cha uhusiano mawasiliano TPDC Maria Mselemu wanajivunia kuwa washindi wa kwanza katika tunzo za serikali
Aidha alisistiza kwamba hiyo ni tuzo ya 5 katika maonyesho ya kimataifa ya biashara( Sabasaba) ni fahari kwao na hakuna aliyeweza kuwapita katika vipindi vyote vitano
" Ni fahari kwetu TPDC katika kupata tuzo katika maonyesho ya 49 ya kimataifa ya biashara na tumezoea kuchua kila mwaka" alisema mselemu
Aliongezea kwamba sio tuzo hiyo tu waliochukua hata kwenye wiki ya mazingira walikuwa washindi ambapo nishati ya gesi asilia imeweza kuondoa hewa ukaa kiasi cha tani laki moja na huko nako tulipata tunzo nyingine, kwa hyo kazi zetu zote tunafanya kwa umakini kwa kuzingatia mazingira ili kufikisha gasi asilia kwa wananchi kama vile katika gari viwanda na matumizi mengineyo.
Pia alisema shughuli zinazofanywa katika banda lao ni kutoa elimu ya namna ya kuhifadhi mazingira kwa kutumia gas asilia





