PURA WAPAMBANA KUTOA AJIRA KWA VIJANA
Na Mwandishi wetu Saba Saba
TPDC imeshiriki kwa 40% ambapo 60% zimebaki kwa watu wa nje" alisema mhandisi
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mkondo wa juu wa petroli Mhandisi wa petroli Charles Sangweni amesema amepongeza maonyesho ya 49 ya kimataifa ya biashara ( Sabasaba) kwa sababu yamekuwa ya kisasa zaidi ( kidigitali ) ukilinganisha na vipindi vya nyuma.
Aidha mhandisi Sangweni aliongeze kwamba ameona mwamko wa wananchi umekuwa mkubwa katika banda la PURA na mswali ambayo yanayoulizwa katika banda lao yamekuwa ya kisomi zaidi ambayo maswali hayo yanaonesha wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa kuhusiana na mafuta na gesi.
Awali kwa leo pia alitembelea banda la PURA na mabanda mengine aliona mwamko mkubwa wa wananchi upo kwenye nishati safi ya kupikia hivyo inaonesha wananchi wamepata elimu ya kutosha kuhusiana na umuhimu wa kutumia nishati safi.
"Tunafahamu kuwa hii agenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kinara wake ni mkuu wetu wa nchi Dkt.Samia Suluhu Hassan na hata Kupitia kwa hiyo inanipa faraja sisi watendaji wake tunafanya kazi kwa vitendo na hatumuangushi" alisema Sangweni
Aliongezea kwamba kazi kubwa ya PURA ni kukusanya data kwa ajiri ya kuangalia upatikanaji wa mafuta,
Kampeni ya kwanza ilifanyika katika maeneo ya bahari kuu 2018 ambapo tulichimba kisima kimoja, na kampeni kubwa ilikuwa katika maeneo ya uchimbaji kati ya wafanyakazi 150 tulikuwa na wafanyakazi 52 kwa mara ya kwanza kutoka ndani ya nchi na wengi walikuwa wamepata uzoefu kutoka nchi mbalimbali na projeti za ndani ya nchi.
" Sasa hivi tunakampeni inayoendelea endapo ipo kwenye maandalizi inaendelea ambapo tutachimba visima vitatu kwa huko Mtwara
Pia alisema kwa kila makampuni kumi ambayo yanawekwa kwenye kazi tutahakikisha zaidi ya makampuni sita yatakuwa ya kitanzania ili kuhakikisha watanzania wanafaidika
