WAZIRI WA ELIMU YA JUU AVUTIWA NA MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA CHUO CHA UFUNDI CHA VETA
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi CPA Antony Kasore Kushoto katika picha akiwa na Waziri wa Elimu ya juu Prof. Pierre Gomez
Na Mwandishi wetu Saba Saba
WAZIRI wa Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Utafiti kutoka Serikali ya Gambia, Prof. Pierre Gomez amevutiwa na Sanaa ya mikono inayofanywa na chuo cha ufundi stadi VETA
ameyasema hayo leo juni 7,2025 katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere ( Sabasaba) wakati alipotembelea banda la veta ndipo alipofurahishwa na ubunifu wa vitendo zaidi kuliko nadharia
" Nilivyopita kwenye banda hili nimependa zaidi Sanaa za mikono zilizotengenezwa kwa ubunifu mkubwa hivyo amefurahishwa sana" alisema Prof. Gomez
Aidha alipenda sana elimu ya Tanzani pamoja na ufundi stadi wa veta unaotolewa unapelekea watu kuendelea kuwa vizuri zaidi kwenye vitendo kuliko nadhalia
Pia aliongezea kwamba kwenye upande wa ubunifu ni mkubwa sana nimeona kwenye bidhaa zilizozalishwa na wanafunzi ni nzuri sana na zinavutia.
Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufudi stadi VETA CPA Antony Kasore amesema ugeni huu umekuja kujifunza mafunzo ya elimu na pia kujione maswala mbalimbali yanayofanyika kuhusiana na sayansi na techolojia pamoja na ubunifu nchini.
" Leo amekuja kwenye maonyesho ya 49 kimataifa ya biashara ( Sabasaba) ili kuangali Taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya elimu jinsi zinazofanya kazi zake na wameweza kuona vitu mbalimbali vinavyofanywa na veta kuanzia kwenye utoaji wa mafunzo, kwenye ubunifu mpaka mwisho wa siku kuweza kuwafundisha watu ujasiliamali" alisema CPA Kasore
Aliongezea kwa kusema mafunzo yanayotolea ni muhimu sana mpaka yanapelekea mtu kujiajiri na kuanza kufanya shughuli za ujasiliamali na pia wameona wafunzo ya veta yalivyojikita kwa vitendo zaidi kuliko nadhalia.


