CCT IMEFANYA MKUTANO MKUU WA 32 JIJINI DODOMA
Na. Wellu Mtaki, Dodoma.
Jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT) imefanya mkutano mkuu wa 32 Jijini Dodoma leo Julai 3,2025 huku Maaskofu,wachungaji pamoja na waumini wa jumuiya hiyo wakihudhuria.
Katika mkutano huo umekuwa na majadiliaono mbalimbali kuhusu Miradi na mipango ya maendeleo yaliyopo chini ya jumuiya hiyo lengo likiwa ni kujumuika pamoja na kufanya tathimini mbalimbali kuhusu Jumuiya hiyo.
Mbali na maeneo yanayoihusu jumuiya pia kwa kushirikiana na serikali wamefanikiwa kutengeneza silabasi za masomo ya dini(Bible knowledge) na Kuwapatia walimu Elimu hiyo ili na wao wapate ujuzi na wakafundishe shuleni.
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Mchungaji Dkt. Moses Matonya amekuwa mmoja wa washiriki walio husika kuandaa vitabu vipya vya mtaala huo ambapo Mpaka sasa vitabu vitatu tayari vimekamilika ,kidato cha Kwanza,cha pili na tatu ambavyo vitaanza kutumika mwakani.
Aidha katibu ameongeza kuwa Vitabu hivyo vitakuwa tayari kwa masomo ya ujuzi wa Biblia kwa wanafunzi wa ngazi za shule ya msingi pamoja na Sekondari kwa upande wa shule za serikali na za kanisa.
Kwenye vitabu hivyo amesisitiza kuwa Moja ya lengo la vitabu hivyo ni kuwa vimeandikwa kwa ustadi kwa lengo la kutoa udini ambapo akisoma mtu yoyote ataelewa na inaonesha ni namna gani taasisi haileti udini.
Katika hatua nyingine katibu ameongeza kuwa walimu wanaosoma masomo ya dini katika vyuo vyao wataajiriwa kwenye shule za dini pamoja na shule za serikali.


