Breaking News

MAVUNDE AKABIDHI SIMU JANJA KWA WENYEVITI WOTE WA MITAA






Na. Wellu Mtaki, Dodoma 


Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde  amekabidhi rasmi vifaa vya kidigitali Simu Janja  (Smartphone) kwa wenyeviti wote wa mitaa ili kuimarisha usikilizaji na utatuzi wa kero za wananchi.

Akikabidhi vifaa hivyo jijini Dodoma amesema kuwa simu hizo zimeunganishwa na mfumo maalum wa kiteknolojia unaowezesha viongozi wa mitaa kuripoti changamoto moja kwa moja kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwa Mbunge hali  ambayo inarahisisha upokeaji na majibu ya haraka kwa matatizo ya wananchi.

"Kupitia mfumo huu, kero yoyote kutoka kata yoyote inaweza kufikishwa ndani ya dakika moja kwa viongozi husika. Ni mfumo wa kwanza wa aina yake hapa Dodoma, na naamini utaboresha kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma kwa wananchi," amesema Mavunde.


Aidha amesema simu janja  hizo  hazitakuwa kwa matumizi ya anasa bali ni nyenzo za kushughulikia matatizo ya wananchi na hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa awali.

Mbali na kugawa vifaa hivyo, Mavunde alichangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa sare za kazi (sakosi) kwa wenyeviti, akisisitiza kuwa anamaliza kipindi chake cha ubunge akiwa ametimiza dhamira ya kuwahudumia wananchi .

Sambamba na Hayo amewataka wananchi Kama kuna mambo akuweza kuyakamilisha, ameomba kushirikiana na atakayekuwa mbunge mpya ili tuendelee kuyafanikisha kwa pamoja," alisema.