WANANCHI WASIFANYE MAKOSA KUCHAGUA KIONGOZI AMBAYE AMESHIDWA KUWAJIBIKA KWENYE MAJIMBO YAO
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Mwanasheria wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) ambaye pia ni Mwanasheria wa Baraza la Machifu Mkoa wa Dodoma Samwel Chimanyi amewataka wananchi wasifanye makosa kuchagua Kiongozi ambaye ameshidwa kuwajibika ipasavyo Katika kipindi Cha madalaka yake bali wahakikishe wanachagua Kiongozi ambaye atawajibika kutatuta changamoto za wananchi kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dodoma wakati wa mahojiano na chombo Cha habari nico Media ambapo Chimanyi amesisitiza kuwepo na uzingatiaji wa kanuni ,taratibu na miongozo inayotokana na Sheria ya uchanguzi kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema viongozi ambao wamepewa idhini na chama chao ila hawakuwajibika ipasavyo kutatua changamoto zilizokuwa ndani ya uwezo wao wasirudishwe madarakani kwani hawajatenda haki kwa wananchi na chama kilichowapa heshima na dhamana ya kupewa madaraka Hayo.
"Wabunge ambao hawakukifanyia kazi Chama hawakukitendea haki Chama kwani walipewa idhini na Chama chao ila wamedhalilisha Chama ,Wananchi wasifanye makosa kuchagua Mbunge ambaye ameshidwa kuwatendea mazuri wananchi na waache kudanganywa kwa ahadi za pesa, Supu bali waangalie mtu mwenye uwezo wa kuongoza kwa haki na busara" amesema Chimanyi
Aidha ameeleza kuwa viongozi waliokuwa na nyadhifa kubwa Serikali kuachia nafasi zao na kwenda kugombea nafasi za Ubunge na udiwani ni haki yao kikatiba hivyo wabunge waliomaliza muda wao waungane nao kwa dhamira njema kwa kuwa kinachoitajika ni kumpata mbunge mwenye uwezo kiutendaji .
"viongozi kuacha nafasi zao na kugombania nafasi za ubunge kwani Sheria inasema kila mwananchi anahaki ya kugombea hivyo wabunge ambao waliokuwepo madarakani na wanaenda kugombea wasiogope wagombea wapya kwenye majimbo yao" amesema Chimanyi
Ikumbukwe kuwa Mwaka huu 2025 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu katika nchi ya Tanzania ambapo kupitia Uchaguzi huo Wananchi hupata fursa ya kuchagua viongozi wao kutokana na sera zao.
