Breaking News

TANI MILIONI 4.87 ZIMEKAMATWA MPAKA SASA

 


Na. Wellu Mtaki, Dodoma 

Serikali Katika kupambana na kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini tangu mwaka 2021 Mpaka sasa zaidi ya tani milioni 4.87 za dawa za kulevya zimekamatwa ikiwa ni juhudi madhubuti katika kuhakikisha tatizo hili linadhibitiwa

Hayo yamesemwa Leo jijini Dodoma na Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati  akihitimisha maadhimisho ya kitaifa ya kupinga vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Amesema kuwa anatambua  kuna mjadala ulioibuka baina ya wachumi na wadau wa kuzuia matumizi ya dawa za kulevya huku wachumi wakidai kuwa zinaleta fedha hali ambayo wameacha kuangalia madhara ya kiafya.

 “Kama tunataka tuwe na kundi la vijana wa Kitanzania mazezeta, basi turuhusu hii biashara. Lakini, Serikali hii tumekataa kwa sababu tunaamini kuwa hiyo mijadala haina tija na hatutairuhusu,” amesema Majaliwa

Aidha ametoa onyo kwa wasambazaji na wauzaji wa dawa za kulevya kuacha vitendo hivyo kwani  Tanzania siyo mahali pa kufanyia biashara hizo.

 “Tanzania siyo mahali salama kwa wauzaji, wasafirishaji na walimaji na hata pia watumiaji wa dawa za kulevya. Tanzania tumeiva na sasa tunaenda kukomesha biashara hii.” amesema Majaliwa.



Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kimataifa Tanzania iko vizuri.

 “Tunakotokea siyo hapa tulipo leo. Wakati ule, tulikuwa tunajulikana kama mapito ya dawa za kulevya. Lakini chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania tumeondoka kwenye doa hilo.


Naye  Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya waziri mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe.Ummy Hamisi Nderiananga ameishukuru serikali  kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye vifaa vya kufanya ukaguzi wa madawa ya kulevya ambapo yameleta matokeo chanya katika nchi ya Tanzania.

Pia Kamishina Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini Aretas Lyimo amesema katika kipindi hiki kupitia ushirikiano wa kimataifa na uongozi madhubuti wa serikali ya awamu ya sita  wamefanikiwa
 tumekamata dawa za kulevya jumla ya kilogramu 2,301,414.94. Kiasi hiki ni kikubwa ikilingalishwa na kilo 2,050,542.73 zilizokamatwa kati ya Juni, 2023 na Mei, 2024. Kuanzia Januari hadi Desemba 2024, jumla ya kilo 2,327,983.8 zilikamatwa ikilinganishwa na kilo 1,965,341 zilizokamatwa kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2023.

Sambamba  na hayo kamishina Jenerali ameeleza kuwa Mamlaka imefanikiwa kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya ambapo watu Zaidi ya milioni 28 wamefikiwa Nchi nzima.

Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya kitaifa ya kupinga vita dhidi ya madawa ya kulevya yameadhimishwa kwa kauli mbiu isemayo " Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya Dawa za kulevya"