Breaking News

RC Makongoro Nyerere Ashinda Safari ya Kombe la Dunia 2026 Kupitia Droo ya CRDB


Na Mwandishi wetu 

Makongoro Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa Julius Nyerere, ameibuka miongoni mwa washindi watatu wa droo ya kampeni ya Kombe la Dunia iliyoandaliwa na CRDB Bank, ushindi uliovutia hisia za wengi kutokana na historia na urithi wa familia hiyo nchini Tanzania.

Makongoro ametangazwa mshindi wa safari ya kwenda kushuhudia michuano ya 2026 FIFA World Cup itakayofanyika nchini United States, Canada na Mexico. Baada ya kupigiwa simu na kuthibitishiwa ushindi wake, Makongoro alijibu kwa kifupi akisema, “Asante sana.”

Washindi wengine wa safari hiyo ni mfanyabiashara maarufu Arun Vithaldas pamoja na Abdulraouf Suleiman, ambao nao watapata nafasi ya kwenda kushuhudia mashindano hayo makubwa ya soka duniani nchini Canada.

Wachambuzi wa masuala ya kijamii na michezo wamesema ushindi huo umeendelea kuonyesha namna ambavyo urithi wa familia ya Nyerere unaendelea kugusa matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo michezo na burudani.

Katika upande wa zawadi za vifaa vya elektroniki, washindi wa televisheni wametangazwa kuwa Amina Kaswala, Lusekelo Michael na Easter Kabakama. Amina Kaswala ameshinda televisheni ya inchi 85, huku washindi wengine wakijinyakulia zawadi mbalimbali kupitia kampeni hiyo ya CRDB Bank ambayo imeendelea kuvutia idadi kubwa ya washiriki nchini.