Breaking News

MCHUNGAJI MASHIMO ASISITIZA UMUHIMU WA AMANI

 


Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam 

Mchungaji Mashimo amesisitiza umuhimu wa kuwa na amani nchini hivyo amewataka Watanzania wote kuilinda na kuitunza tunu hiyo.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 23,2025 ambapo aliwataka viongozi wote wa dini kuhubiri umuhimu wa amani.

Leo hii pia nilipata nafasi ya kumsikiliza mzee wetu, mtumishi wa Mungu na waziri mstaafu, mzee Warioba. Alizungumza kwa uchungu mkubwa kuhusu yaliyotokea Oktoba 2025, akieleza kuwa  Kauli yake imenigusa sana, na imenifanya nitafakari kwa kina kuhusu hali ya taifa letu. Ni wazi kuwa tumepitia maumivu mengi kama taifa, na hakuna Mtanzania ambaye hajaguswa na huzuni ya namna moja au nyingine.

"Katika kipindi hiki, tunahitaji kusimama pamoja kama viongozi wa dini, wazee wa taifa, na raia wenye mapenzi mema. Tuwe na msimamo wa pamoja wa kulijenga taifa letu na kulirudisha katika hali ya faraja maumivu ya zamani yasitumike kama chachu ya chuki au mgawanyiko badala yake, tuyatumie kama msingi wa kuimarisha mshikamano na kuponya vidonda vya taifa letu" amesema Mchungaji Mashimo 

Katika hatua nyingine Mchungaji mashimo amepongeza juhudi za serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto zilizojitokeza, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa tume maalum ya kuchunguza matukio hayo. Ni busara tukaisubiri tume hiyo itoe majibu yake. Iwapo majibu hayo hayatakidhi matarajio ya Watanzania, basi tuna haki ya kuuliza, kutoa maoni, na kuhoji kwa njia ya amani. Lakini kwa sasa, tunapokaribia sikukuu ya Krismasi, naomba viongozi wa dini wote tushirikiane kulinda amani ya nchi yetu.

Mchungaji mashimo alisema huu sio wakati wa kuendeleza maumivu wala kuhamasisha chuki bali ni wakati wa kuwa faraja kwa taifa letu hivyo viongozi wa makanisa yote—Roman Catholic, KKKT, TAG, Moravian, Wasabato, Wapentekoste na wengine wote—tushikamane kama kitu kimoja. Hakuna serikali iliyo kamilifu duniani, lakini kwa hekima na mshikamano, tunaweza kuijenga Tanzania yenye haki, amani na matumaini.

Mchungaji Mashimo ametoa wito kwa  viongozi wa dini kuhubiri amani na utulivu sanjari na  wanasiasa na viongozi wa serikali nao wafanye hivyo. Utulivu ni msingi wa maendeleo na ustawi wa taifa. Yesu Kristo awe nuru yetu, na Krismasi hii iwe mwanzo mpya wa mshikamano na upendo.

 Wito kwa mtumishi wa Mungu na kiongozi wa Kanisa la National Christian Assemblies, ninazungumza kwa dhamira safi. Kuna mengi nitakayozungumza siku zijazo, lakini leo nafungua ukurasa mpya wa mazungumzo ya kweli, ya haki, na ya kujenga. Mungu ibariki Tanzania. Mungu awabariki viongozi wetu. Na Mungu awabariki Watanzania wote.