Tanzania Yalenga Kuzalisha Megawati 10,000 za Umeme Ifikapo 2030 – Maonesho ya Tisa ya Nishati ya Jua Yafunguliwa
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati, Emilian Nyanda amesema kuwa Tanzania inalenga kuzalisha hadi megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2030 ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi, kijamii na maendeleo ya viwanda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Tisa ya Nishati ya Jua yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Nyanda alieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa *Dira ya Maendeleo ya 2050*, inayolenga kuhakikisha taifa linakuwa na umeme wa kutosha kwa maendeleo endelevu.
“Leo hii Tanzania imeandaa mpango wa matumizi ya nishati safi. Hii ni fursa kwa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika matumizi ya teknolojia za nishati mbadala,” alisema Nyanda.
Aliongeza kuwa serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya sera ya Nishati ya mwaka 2025 inayolenga kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya nishati jadidifu.
Kwa upande wake, Oscar KisangaMkurugenzi Mkuu wa Chemba ya Biashara Tanzania, alisema kuwa maonesho hayo yamewaleta pamoja wadau kutoka mataifa mbalimbali, na kutoa fursa kwa sekta binafsi kuonyesha bidhaa na teknolojia wanazozalisha zinazohusiana na nishati.
“Wenzetu kutoka Ujerumani wamekuja na teknolojia ya kisasa katika sekta ya nishati ya jua. Ni wakati wa Watanzania kuchangamkia fursa hizi,” alisema Kisanga.
Aidha, Kisanga alitoa shukrani kwa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara, yanayowezesha ushirikiano wa kimataifa na kukuza sekta ya nishati nchini.
Hata hivyo kwa upande wake afisa maendeleo ya biashara wa kampuni ya InSolare ndugu Ajay Ramdev amesema kupitia maonyesho hayo ya tisa ya jua alisema wanauwezo wa kutatua na kutoa huduma katika uuzaji wa vifaa vya nishati kama vile sola( solar PV Module),Green Hydrogen pamoja na Renewable energy.
" Ni miongoni mwa kamapuni ambayo inafanya vizuri katika nchi ya India mpaka ikapelekea kupata tuzo nchini India hivyo tunataka kuungana na nchi ya Tanzania ( joint venture) ili kuweza kuungana katika kufanya biashara ya pamoja ya kushirikiana hivyo itapelekea kuzidi kukua katika matumizi ya nishati" alisema Ajay Ramdev
Maonesho hayo ya nishati ya jua yamehudhuriwa na washiriki kutoka nchi 25 ikiwemo banda la InSolare washiriki hawa ni kutoka nchi ya India nao walifurahia katika ushiriki kwenye maonyesho ya expo ya nishati ya jua ya tisa hivyo wakijadili na kuonyesha maendeleo ya teknolojia ya nishati ya jua ambayo yatafanyika ndani ya siku tatu kuanzia tarehe 08 mpaka 10 Oktoba 2025.






