Breaking News

Kura za Maoni za CIP-Africa Zafichua Mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025


Na Hawa Ismail- Dar es Salaam 

Kituo cha Sera za Kimataifa-Afrika (Centre for International Policy-Africa, CIP-Africa) kimetoa matokeo ya utafiti wa kisayansi kuhusu mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Utafiti huo ulifanyika kati ya Septemba 30 hadi Oktoba 5, 2025, ukihusisha washiriki 1,976 kutoka mikoa 20 nchini Tanzania. Washiriki hao walikuwa na uwiano sawa wa kijinsia—wanaume 988 na wanawake 988—na asilimia 29 walikuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 56.


Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 22, 2025, Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa CIP, Thabit Mlangi, alieleza kuwa vyama 18 vya siasa vimefanikiwa kusimamisha wagombea katika nafasi za urais, ubunge na udiwani. Miongoni mwa vyama hivyo ni CCM, ACT-Wazalendo, CUF, Chaumma, SAU, UDP, Makini, NLD, NCCR-Mageuzi, NRA, AAFP, UPDP, ADA-TADEA, D, TLP, CCK, ADC na DP.


- Asilimia 81 ya washiriki walijitambulisha kuwa wanafuatilia siasa za nchini.

- Wanaume waliongoza kwa ufuatiliaji kwa asilimia 57, wanawake wakichangia asilimia 43.

- Kwa ngazi ya elimu: msingi (19%), sekondari (55%), na elimu ya juu (26%).


 Aidha Vipaumbele vya Wananchi kwa Rais Ajaye pamoja na 

- Maji: 78%

- Elimu: 78%

- Miundombinu: 69%

- Kupambana na rushwa: 60%


Utafiti ulifanyika katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja, Kigoma, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Tabora na Tanga.


- Asilimia 83 ya washiriki wamethibitisha kuwa watapiga kura Oktoba 29.

- Kura za maoni zinaonyesha asilimia 84.5 wanampendelea mgombea wa CCM.

- Asilimia 8 walibainisha kuwa kura yao ni siri.


 CIP-Africa imeishukuru serikali kuu na za mitaa kwa kuunga mkono utafiti huo, na kuwasihi wananchi wajitokeze kupiga kura kwa amani na utulivu, wakikumbuka kauli mbiu: _“Kuna maisha baada ya uchaguzi.”