Breaking News

KAMPENI ZA ACT WAZALENDO: AHADI ZA MAGEUZI KWA WANANCHI WA ILALA, KARIAKOO NA GEREZANI

  

Katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, wagombea wa chama cha ACT Wazalendo wameendelea kutoa ahadi mbalimbali kwa wananchi wa Dar es Salaam, wakilenga kuboresha maisha ya watu wa kawaida kupitia sera za uwajibikaji na usawa.

Friday Yachitwi (Kalulu) – Mgombea Ubunge Jimbo la Ilala

Mgombea huyo ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wamachinga, akisisitiza kuwa atatetea haki za kina mama wajawazito ili wasitozwe fedha wanapojifungua.

Aidha, Kalulu amesema atasimamia kwa karibu masuala ya kodi na ushuru, akilenga kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa.

“Wafanya biashara nitaenda kusimamia kodi pamoja na miundombinu mibovu kwa kutengeneza mitaro ya kupitisha maji machafu,” amesema Kalulu.


Vilevile, ameahidi kuhakikisha bima za afya zinapatikana kwa usawa kwa watu wote, na kutoa mashine za EFD bila malipo ili kurahisisha ufuatiliaji wa mapato.

Katika mkutano wa kampeni uliofanyika jijini Dar es Salaam, Bombwe amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi.

Ameahidi kuboresha barabara za Kariakoo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, akilenga kurahisisha shughuli za biashara na usafiri katika eneo hilo maarufu kwa biashara.

Gogo ameweka wazi nia yake ya kupunguza gharama za ushuru wa takataka za majumbani na ushuru wa kuegesha magari, akisema bei hizo zinapaswa kuendana na hali halisi ya wananchi.

 “Nitahakikisha barabara za Gerezani zinakuwa za kiwango cha lami na kodi za jengo zilipwe na wamiliki wa majengo,” amesema Gogo.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Maharagande, amesema chama hicho kinaamini katika sera ya _taifa la wote kwa maslahi ya wote_, na endapo watapewa ridhaa ya kuongoza, watasimamia maendeleo ya taifa kwa uwazi na uwajibikaji.