Breaking News

Kampuni ya Mr Bontel Yazindua Simu za Kisasa Zenye Chaji Inayodumu Miezi Mitatu

Kampuni ya Mr Bontel imeleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano kwa kuzindua simu za kijanja zenye uwezo wa kuhifadhi chaji kwa muda wa kuanzia mwezi mmoja hadi miezi mitatu, hatua inayolenga kuwasaidia watumiaji wanaokumbwa na changamoto za umeme na mtandao.

Katika maadhimisho ya miaka 22 ya wakandarasi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, mfanyakazi wa kampuni hiyo Bi Joyce Fikiri alieleza kuwa bidhaa zao zinapatikana kwa bei nafuu sana, zikiwemo simu za mezani, simu za mkononi, redio, pasi za umeme, taa za sola, power banki, na chaja za simu.

 “Tunayo simu ya mezani ambazo ni bei nafuu sana na unaweza ukazitumia kwa matumizi ya nyumbani au ofisini. Pia tunazo simu zinazofanya kazi hata maeneo ambayo mtandao haushiki, na unaweza kuzitumia kama power bank kuchaji simu nyingine,” alisema Bi Joyce Fikiri.

Kwa upande wake, Bi Juliana Mgumbuka aliongeza kuwa Mr Bontel pia wanauza mashine za kunyolea watoto kwa bei ya shilingi 10,000 pamoja na waya wa kuchajia (USB), jambo linalowafanya kuwa chaguo bora kwa familia na wafanyabiashara wadogo.

Mr Bontel wanapatikana katika kila kona ya Tanzania, wakitoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa bei nafuu, na hivyo kuendelea kujizolea umaarufu miongoni mwa Watanzania wanaotafuta suluhisho la kudumu katika teknolojia ya mawasiliano na vifaa vya nyumbani.