🟣 HALOPESA YAJA NA BONASI – TAMBA NA BONASI KWA KUFANYA MIAMALA
Huduma ya kifedha ya Halotel, _Halopesa_, imezindua rasmi kampeni mpya iitwayo *"Tamba na Bonasi"*, sambamba na utambulisho wa msaidizi wa kidigitali anayefahamika kama *Mr. Bonasi*, ambaye atakuwa sura rasmi ya kampeni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, tarehe 19 Septemba 2025, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Halotel, *Happy Mzena*, alieleza kuwa kupitia kampeni hii, wateja wa Halopesa watapata fursa ya kujishindia bonasi kabambe kwa kufanya miamala mbalimbali. Miamala hiyo ni pamoja na kutoa pesa, kulipia bidhaa, na kununua umeme ( _LUKU_), ambapo wateja wanaweza kujishindia hadi *shilingi milioni mbili (2,000,000)* pesa taslimu kupitia droo za kila siku, kila wiki, na kila mwezi.
“Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wetu wa kuendelea kuwapa wateja thamani zaidi. Mr. Bonasi siyo tu nembo ya kampeni, bali ni jukwaa la kidigitali la zawadi linaloleta msisimko katika kila muamala. Lengo letu ni kuifanya kila huduma ya Halopesa kuwa fursa ya ushindi kwa wateja wetu,” alisema Happy Mzena.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Halopesa, *Aidat Lwiza*, alisisitiza kuwa kampeni hii imebuniwa kwa ubunifu mkubwa na inaleta thamani halisi kwa wateja. Aliongeza kuwa Halopesa inaendelea kuwa kinara sokoni kwa kutoa makato nafuu zaidi ukilinganisha na huduma nyingine, huku ikijivunia mtandao mpana wa mawakala na maduka ya Halotel nchi nzima.
“Kupitia kampeni hii, maelfu ya wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi na kuwaka na Mr. Bonasi kila siku, wiki, na mwezi. Tunawakaribisha Watanzania wote kujiunga na Halopesa, kwani kwa sasa kila muamala siyo tu njia ya kutuma au kupokea fedha, bali ni hatua moja kuelekea ushindi,” alisema Aidat.
Aidat alihitimisha kwa kuwakumbusha wateja kuwa taarifa zote za ushindi zitatumwa kupitia ujumbe rasmi wenye jina la _Halopesa_, na simu zozote kutoka Halopesa zitatoka kupitia namba ya huduma kwa wateja *"100"*. Alitoa wito kwa wateja kuwa waangalifu na kutotoa taarifa binafsi kwa namba au watu wasiothibitishwa. Kwa msaada zaidi, wateja wanahimizwa kutembelea maduka ya Halotel au kupiga simu bure kupitia namba hiyo ya huduma.




