Breaking News

SANGA AAHIDI KUIJENGA KIGAMBONI

Mgombea mteule jimbo la Kigamboni, Haran Sanga, alipopewa nafasi ya kuwasalimia wapigakura wake, 31 Agosti 2025, uwanja wa Sokoine Temeke


Na Kelvin Kijo

"Mgombea Mteule wa Jimbo la Kigamboni, Ndugu Haran Sanga, amepokea rasmi Ilani ya CCM ya kampeni zake tarehe 31 Agosti 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa wabunge wa majimbo 12 na madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza kwa msisitizo, Sanga alieleza kuwa kipaumbele chake kikuu ni barabara.

“Cha kwanza ni barabara, cha pili ni barabara na cha tatu ni barabara. Huduma za kijamii zote zimeshaainishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),” alisema Sanga.

Katika uzinduzi mkuu wa kampeni za CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliwaahidi wananchi kuwa huduma zote za kijamii zitaimarishwa na kuwekwa sawa ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa tena.

Sanga amewaalika wananchi wa Kigamboni kushiriki katika mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni ya jimbo lake, utakaofanyika tarehe 6 Septemba 2025, Kata ya Mwasonga.

“Nitafafanua kwa kina Ilani ya CCM, hususan katika jimbo la Kigamboni,” aliongeza Sanga