Breaking News

YASHANGAZA MKURUGEZI MKUU COPRA ALICHOKISEMA

 



Na. Wellu Mtaki, Dodoma 

Serikali Katika kuhakikisha kilimo kinasonga mbele  imeweka juhudi kubwa katika sekta ya mazao na kusimamiwa ipasavyo, hususan zao la mahindi ambalo kwa muda mrefu limekosa msimamizi wa moja kwa moja


Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Irene Mlola katika warsha ya zao la mahindi kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma huku akisema  kuanzishwa kwa COPRA ni sehemu ya mpango madhubuti wa serikali wa kuweka mazingira rafiki kwa biashara ya mazao nchini.

Aidha ameeleza kuwa  suala nyeti la ubora wa mazao  COPRA inalichukulia kwa uzito mkubwa suala la ubora kwani ndilo linaloamua ushindani wa mazao ya Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje.
 



"Bila udhibiti wa ubora, tunaweza kuzalisha kwa wingi lakini tukakosa masoko. Kupitia kanuni na miongozo ya ubora, tunahakikisha mazao kama mahindi yanakidhi viwango vya soko,” amesema 


Sambamba na Hayo amebainisha kuwa taasisi hiyo kwa sasa inafanya kazi kwa karibu na NFRA katika usajili wa wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani kama vile wanunuzi, wasindikaji, wasafirishaji, na wamiliki wa maghala au maeneo ya biashara ya mazao ikiwa Lengo kuu ni kuhakikisha taarifa hizi zinatumika kusimamia sekta kuanzia shambani hadi sokoni.


Ikumbukwe maonesho ya nanenane  inabebwa na kauli mbiu isemayo "Chagua viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo na Ufugaji na Uvuvi 2025".