TCRA yafundisha wanablogi kujiandaa na Uchaguzi Mkuu 2025
| Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akiwasisitiza jambo wanablogi wakati wa mafunzo, 11 Agosti 2025 Dar es Salaam |
Na Kelvin Kijo - Dar es Salaam
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya mafunzo maalum kwa wamiliki na waandishi wa blogi tarehe 11 Agosti, ili kuwaandaa kuripoti matukio yote ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa uwazi na bila kuegemea upande wowote.
Akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, amewaelekeza wanablogi kuzingatia mambo manne muhimu wakati wa uchaguzi ili kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza.
“Mnapaswa kutoa elimu kwa umma, taarifa za mchakato wa uchaguzi, kuwafahamisha wapiga kura ratiba na taarifa muhimu kutoka kwa tume huru ya Uchaguzi, pamoja na kuwa kipaza sauti cha kutangaza matokeo ya uchaguzi,” amesema Kisaka.