Breaking News

Orodha ya waandishi wa habari waliouawa katika vita vya Hamas na Israel

 


Mavazi ya mwandishi habari Muhammad Sobh aliyeuwa na mashambulizi ya Israel akiwa mbele ya hospitali ya Gaza
    • Author,Laila Bashar Al-Kloub
    • Nafasi,BBC

Idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel kwenye mji wa Gaza inazidi 14,128, wakiwemo watoto zaidi ya 5,000, kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza, huku Israel ikitangaza idadi yake ya vifo ni 1,200.

Vita vinavyoendelea vimechukua maisha ya watu wengi - wakiwemo waandishi wa habari. Zaidi ya waandishi wa habari 53 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameuawa, kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari.

Kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari, waandishi wa habari 53 waliuawa kuanzia Novemba 7 hadi 22: Wapalestina 46, Waisraeli wanne, Walebanon watatu, na waandishi wa habari 11 waliripotiwa kujeruhiwa, watatu walipotea, na wengine 18 waliwekwa kizuizini.