Breaking News

NJAMASI CHIWANGA NYOTA YAKE YANGARA KATIKA KAMPENI KWA WAJUMBE WA JIMBO LA MPWAPWA

 


NA. Barnabas kisengi , Mpwapwa 

Mpwapwa mbio za kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mpwapwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kushika kasi, baada ya kutangazwa kwa majina ya wagombea saba waliopitishwa na Kamati Kuu ya chama cha Mapinduzi 


Wagombea hao wameanza kujinadi mbele ya wajumbe wa CCM katika kata mbalimbali za jimbo hilo, leo kwa mwaka,2025 wakiainisha dira na mikakati yao ya kuleta maendeleo endapo watapata ridhaa.


Kampeni za ndani ya chama cha Mapinduzi CCM zilianza Julai 30, 2025  na zitahitimishwa Agost 3 2025.


 Ambapo Njamasii Chiwanga aliyekuwa mkulugenzi wa Mazingira kutoka kampuni ya Lead foundation (Kisiki hai) wilayani mpwapwa ni miongoni mwa watia nia saba waliochaguliwa kupeperusha bendala ya chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Mpwapwa.


Katika hotuba yake kwa wajumbe Njamasii Chiwanga ameainisha vipaumbele vyake vinavyolenga kutatua kero za msingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, akisisitiza dhamira ya utumishi uliotukuka na ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi ya maendeleo.


Njamasii Chiwanga amesema kuwa Wajumbe wakimoatia ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la Mpwapwa atahakikisha wanatekeleza vizuri ilani ya Chama cha Mapinduzi katika vipao mbele vilivyopo katika jimbo hilo


" Nitahakikisha ninasimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ikiwepo mikopo kwa Makundi ya wanawake,vijana,Wazee na makundi ya watu wenye ulemavu"amesema chiwanga


Watia nia saba waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ya ubunge katika jimbo la Mpwapwa Njamasii Chiwanga naye ametia nia Njamasii Chiwanga ni mtoto wa askofu Mstaafu wa kanisa la Anglican na Baba yake pia aliwahi kuhudumu kamaewaziri wa elimu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya kwanza na pili.


Mbio hizo za kusaka kura za maoni utahitimishwa leo Jumapili na kesho Agost 4 kutafanyika zoezi la kupigiwa kura za maoni za chama cha Mapinduzi.