CMSA WACHOCHEA MAENDELEO KWA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA FEDHA
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na dhamana ( CMSA ) inachochea maendeleo kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha kutoka kwa wawekezaji na kupeleka kwenye uzalishaji .
Kauli hiyo ameitoa Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma Charles Shirima wakati azungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nanenane jijini Dodoma Leo Agost 3 ,2025 huku akiwaasa wananchi kutambua umuhimu wa Mamlaka hiyo Ili kujiinua kiuchumi.
Aidha amesema kuwa CMSA ni njia sahihi ya kuwekeza kwani inasaidia kuepuka hatari za kupoteza fedha kwa kutapeliwa kwa kuambiwa watapata faida kubwa kumbe tofauti na matokeo.
Pia Mamlaka inashauri Wananchi na wawekezaji walio na Adhima ya kuanzisha mfuko wa Uwekezaji kuwa na waraka wa kisheria wa kuundwa kikundi ( Katiba) pamoja na mpango kazi .
Sambamba na Hayo Mamlaka inatoa hamasa kwa wanafunzi wa vyuo kwa kuanzisha mashindano ambayo yatampa Elimu mwanafunzi huyo na kunisaidia kuwekeza kupitia ushindi unaotakana na shindano Hilo.
Ikumbukwe kuwa maonesho ya 32 ya nanenane walifunguliwa Agost 1,2025 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango .


