CAMGAS: Gesi Kidogo Mapishi Mengi
Na mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa CAMGAS, ambaye pia ni mtaalamu wa nishati safi, Bw. Sadiq Abri, leo tarehe 26 Agosti amesema mashindano ya upishi ya Ngome ya Mama Samia yamelenga kulinda mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
“Tumezingatia afya za Watanzania, hasa mama zetu wanaotumia kuni na kutembea umbali mrefu kutafuta kuni. Ni hatari kwa afya na mazingira,” alisema Bw. Sadiq.
Katika hafla hiyo, Kampuni ya Camel Oil (Amsons Group) iliendelea kuitambulisha rasmi bidhaa yake mpya ya CAMGAS, inayopatikana katika mitungi ya ukubwa tofauti; Ndogo (6 Kg), Kati (9, 15 Kg), na Kubwa (30 Kg).
Sambamba na hilo, kampuni pia ilizindua unga wa ngano wa Camel, unaopatikana kuanzia ujazo wa kilo 1.
Mafunzo ya Usalama wa Gesi yakafanyika ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa CAMGAS, elimu maalum ilitolewa na Afisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto Kinondoni, Afande Aman Hassan.
Aman alifafanua hatua za tahadhari katika matumizi ya mitungi ya gesi, ikiwemo:
- Kutowasha simu karibu na gesi.
- Kwanza kuwasha kiberiti kisha kufungua gesi.
- Umuhimu wa kumiliki fire extinguisher majumbani.
- Kutumia kitambaa chenye maji kuzima moto jikoni badala ya karatasi au vifaa vikavu.
Aidha, alikumbusha umuhimu wa kujua namba ya dharura ya Zimamoto na Uokoaji:
“Wakati wa janga la moto, piga bure kwa haraka namba 114,” alisema Afande Hassan.
Hafla hii ilifanyika katika Ukumbi wa Msasani Beach, Kata ya Kawe Dar es Salaam, na ilihudhuriwa na washiriki mbalimbali waliopata fursa ya kujifunza na kushiriki katika mashindano hayo ya upishi.
![]() |
| Afande Aman Hassan akielekeza namna bora ya kutumia mitungi wa gesi na wakati wa kuzima moto |
![]() |
| Sadiq Abri Mkurugenzi Mkuu CAMGAS |
![]() |
| Mama Ntilie katika mashindano ya upishi mbalimbali kwa kutumia unga wa ngano kutoka Camel |
![]() |
| Sophia Simba akishangilia na mama ntilie wa Kata ya Kawe |





