Breaking News

ZAIDI YA SHILLING BILIONI 146.3 ZIMETOLEWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KAGERA


 Na. Wellu Mtaki, Dodoma 
Serikali Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya Bora Katika Mkoa wa Kagera zaidi ya Shilingi Bilioni 146.3 zimetolewa na serikali kwa ajiri ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka.

Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya serikali ya awamu ya sika Katika Mkoa wa huo.

Amesema vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka hadi 336 kutoka vituo 249 sawa na Ongezeko la vituo vipya 87 ikiwa  Hospitali  11 mpya za Wilaya 8 na huduma za kibingwa mpya 5 ikiwemo Upasuaji wa pua, koo na
 masikio, mifupa na magonjwa ya ndani .

"Vituo vya afya kutoka 29 hadi 42, vipya 13.zahanati kutoka 217 hadi 283, mpya 6
Huduma za kibingwa mpya 5 (Upasuaji wa pua, koo na masikio, mifupa na magonjwa ya ndani) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa zimeongezwa,hivyo wagonjwa wa rufaa waliotibiwa ndani ya Mkoa wameongezeka hadi kufikia 478,002 ikilinganishwa na 128,305. Ongezeko la wagonjwa wa rufaa 349,697 (273%) ambao wangetibiwa nje ya Mkoa"amesema Mwassa.


Aidha ameeleza kuwa Shilingi Bilioni. 117.9 zimetolewa  kwa ajili ya  miundombinu ya barabara katika Mkoa huo  ambapo Ujenzi daraja la Kitengule lenye upana wa mita 140 na barabara unganishi Wilaya ya Missenyi na Karagwe za km 18 kwa gharama ya Shilingi Bilioni. 31.55 .

"Idadi ya madaraja kutoka 458 hadi 468  Baadhi ya miradi mikubwa ya barabara iliyotekelezwa: -Ujenzi daraja la Kitengule lenye upana wa mita 140 na barabara unganishi Wilaya ya Missenyi na Karagwe za km 18 kwa gharama ya Tshs Bil. 31.55 – umekamilika.Ukarabati barabara ya Lusahunga hadi Rusumo (km 92) kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Tshs. 

Bil. 153.56 – umefikia 19%Ujenzi wa barabara ya Bugene – Kasulo (BENACO) – Kumunazi (km 128.5) kwa gharama ya Tshs. Bil. 92.84 - umefikia 35%.Upanuzi wa barabara njia nne Rwamishenye - Bandarini (Bukoba) kwa gharama ya Tshs. Bil. 5.311 - umefikia 44%.Ujenzi wa madaraja makubwa matano " amesema Mwassa 

Pia amesema Katika kuendeleza uboreshaji wa Bandari bukoba na kemondo shilling Bilioni 26.241 zimetolewa kwa ajili ya  Uboreshaji wa  majengo ya abiria ili kuhudumia abiria wengi zaidi, kuongeza eneo la maegesho ya magari, kuongeza urefu wa magati na kina cha maji. 

"Uboreshaji Bandari (Bukoba na Kemondo), Jumla ya Tshs Bil. 26.241 zimetolewa Uboreshaji unahusisha majengo ya abiria ili kuhudumia abiria wengi zaidi, kuongeza eneo la maegesho ya magari, kuongeza urefu wa magati na kina cha maji. Utekelezaji, bandari ya Kemondo ni sawa na 100% na Bukoba ni 99%. " Amesema Mwassa