ALIYEKUWA DIWANI TEMEKE MH. MWAKYEMBE AJITOSA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE
Na Hawa lsmail
Aliyekuwa Diwani wa kata ya mtoni Bernard Mwakyembe ajitosa ubunge jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam
Leo 2 julai 2025 aliyekuwa diwani wa kata ya mtoni Bernard Mwakyembe amerudisha fomu ya kuomba ridhaa kupata nafasi ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) katika ofisi za CCM wilaya ya Temeke.
Aidha kwa upande wake Mwakyembe ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge jimbo la Temeke ili kuweza kusimamia mikopo ya kina mama, vijana na walemavu inayotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Kwa Temeke bajeti ni Billioni 53 sawa na 10% hizi pesa zinatakiwa ziwasaidie vijana 4%, wanawake 4% na 2% walemavu mimi kama kijana nikipata ridhaa kupitia chama changu cha CCM naenda kusimamia wapate mikopo" alisema Mwakyembe
Hata hivyo Katibu wa wilaya ya Temeke wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel George Sai alisema wagombea wote wa majimbo matatu yaani Temeke, Mbagala na Chamazi wote wamerudisha fomu hakuna asiyerudisha.
Aidha katibu wa CCM Daniel George alisema kwa jimbo la Temeke wamejitokeza watia nia 25, jimbo la mbagala 25 na jimbo la chamazi 15.



