WIZARA YA MAMBO YA NDANI NA SADC WAKUBALIANA KUKABILINA NA MAJANGILI WA WANYAMAPORI
Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi na Mwenyekiti wa mkutano wa SADC Dkt. Maduhu Isaac Kazi wamekubaliana kukabiliana na majangili wa wanyamapori kwa kushirikiana ili wawe salama
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo 26 juni 2025 katika kikao hicho walisistiza zaidi utunzwaji wa wanyamapori katika sehemu zote za hifadhi za wanyama pori.
"Kwenye upande wa wanyamapori pori kuna makubaliano mbalimbali ambayo yamefikiwa ambayo yanahusiana namna ya kukabiliana na majangili ambao wanaingia kwenye maeneo ya wanyamapori wetu hivyo tunahakikisha tunafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha wanyamapori wetu wanakuwa salama" alisema Dkt. Maduhu
Aidha kikao hicho pia walijadiliana kuhusu uhamiaji, na huduma kwa wakimbizi ili kuhimalisha ulinzi na usalama katika nchi hizo za jumuiya ya SADC
Aidha kwa upande wahamiaji wameweka taratibu nzuri kwa watu wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kupata shida yoyote
Pia kwa upande wa wakimbizi wanaotoka nchi moja kwenda nchi nyingine wanasaidiwa ili kuweza kufika na kuwarudisha kwenye nchi zao wakiwa salama.
"Tutakuwa tunawapa ushirikiano wa kudumu kwa wakimbizi wanaohama na tunaangalia suluhisho la kudumu kwa wakimbizi ili kuweza kurudi kwenye nchi zao na kuendelea na kazi zao" alisema maduhu
Hata hivyo mkutano huo umeudhuriwa na nchi zaidi ya 10 ikiwemo Tanzania, Malawi,Mozambique, Congo, Namibia, Portuguese, Angola, Afrika Kusini.

