Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa waitaka Tanzania kusitisha vitendo vya kutoweka kwa wapinzani
Habari: BBC
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha mara moja vitendo vya kutoweka kwa wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.
"Kuminya uhuru wa vyombo vya habari na kutisha waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu, ni jambo lisilokubalika.
''Tunasikitishwa na ripoti za ukandamizaji kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania mwezi Oktoba," wataalamu hao walisema.
Ripoti hiyo inafuatia kutekwa kwa watetezi wawili wa haki za binadamu na waandishi wa habari, Boniface Mwangi kutoka Kenya na Agather Atuhaire kutoka Uganda, jijini Dar es Salaam tarehe 19 Mei 2025.
