SERIKALI IMEISHUKURU BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KWA KUWAPA MKOPO WA BEI NAFUU
Na. Wellu Mtaki, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameipongeza na kuishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kuipatia serikali mkopo wa bei nafuu.
Dkt Samia ameyasema hayo Leo June 14 katikati eneo la Nala lililopo Jijini Dodoma mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya mzunguko nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3.
Mheshimiwa Rais ameongeza kuwa mkopo huo kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika katika utekelezaji wa mradi wa Barabara hiyo ni Shilingi bilioni 489 na milioni 982 ambayo ni Sawa na asilimia 85 huku serikali ya Tanzania ikitoa Shilingi bilioni 90 sawa na asilimia 15.
" Tunaishukuru sana Benki ya Maendeleo ya Afrika na nimefurahi kuwa leo Rais wa Benki yupo nasi kujionea kazi iliyofanyika na inayoendelea kufanyika na namna ambavyo kazi hii inaenda kuimarisha uchumi wa Nchi na kustawisha maisha ya watu" amesema Dkt. Samia
Naye Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Akinwumi Adesina ametoa shukurani zake kwa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake madhubuti na jitihada zake katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu mikubwa na ya kimkakati .
"Dhamira ya Benki ya Maendeleo ya Afrika ni kuendelea kuwaMbia mkubwa kwa Tanzania katika utekelezaji wa miradi hii hususani katika kuendeleza shoroba zinazo anzia Bandari ya Dar es salaam na kuunganisha Nchi nane zisizo na mlango wa Bandari ". Amesema Adesina.
Pia Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amempongeza mheshimiwa Rais na serikali kwa kuendelea kuweka mkazo katika miradi ya Uchukuzi ambayo imeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi Nchini Tanzania.
Prof.Mbarawa ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne serikali imeendelea kutoa fedha ambazo zimewezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta ya Uchukuzi ikiwemo ununuzi wa Ndege za kampuni ya Ndege ya ATCL ambayo kufikia Sasa Kuna ndege 16,uendeshaji wa viwanja vya Ndege, pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).
Mbali na Waziri Mbarawa naye waziri wa ujenzi mheshimiwa Abdalah Ulega amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 kuwa maelekezo ya Rais wataweka Taa za Barabarani mwanzo Mpaka Mwisho.
Mwisho mheshimiwa Rais Dkt Samia ameziomba wizara ya Uchukuzi pamoja na wizara ya ujenzi kuhakikisha kazi ya ukarabati wa Miundo mbinu ya Barabara, Reli na viwanja vya Ndege inatekelezwa kwa viwango vilivyokusudiwa na kuwaasa wananchi wa Dodoma kupamba Barabara hiyo kwa kupanda zabibu pamoja na zao la alizeti na kuhakikisha wanaitunza Miundo mbinu hiyo.


